Sambaza....

EMMANUEL Amunike alipofika tu Tanzania na kupewa kazi ya kuinoa Stars, mchezaji wa kwanza kumuengua alikuwa Erasto- akaenda Cape Verde akachapwa 3-0. Tukamshinikiza ‘tunamtaka Erasto’ akamrejesha, Stars ikashinda 2-0 vs Cape Verde katika ‘rematch’. Kiungo huyo mkali akafungua ‘pazia’ katika ushindi ulioipeleka Stars katika michuano hii ya CAN katika ushindi wa 3-0 vs Uganda mwezi Machi.

Nadhani Amunike ana tatizo binafsi na Erasto kama sivyo aambiwe wazi Watanzania ‘Tunamkata Erasto’ kikosi cha kwanza Stars hata kama itapoteza mechi. Unamuachaje benchi mchezaji aliyekamilika kwa michuano kama huyu? Kuwapanga vijana kama Feisal Salum na kumuacha nje Erasto aliye katika utimamu wa kimwili au kiakili ni kumkosea heshima.

Nyoni akiongoza msafara wa kushangiilia goli lake dhidi ya Uganda

Erasto anajulikana kwa wapenzi wengi wa soka nchini kwa uwezo wake wa kuituliza timu inaposhambuliwa na upangaji wa mashambulizi, ana nguvu na uwezo wa kupora mipira . baada ya kuchemka vibaya kwa Feisal na kushindwa kufanya vizuri kwa Mudathir Yahya na Himid Mao ni wazi nafasi ya Erasto kuanza dhidi ya Kenya ipo wazi na si kwa sababu ya upendeleo bali uwezo alionao.

Na uzoefu wa kuchezea Stars kwa miaka Zaidi ya 13 sasa, nguvu, ufundi na uwezo wa juu katika kuusoma mchezo. Amunike amekuwa na makossa mengi katika upangaji wa kikosi chake tangu wakati wa kufuzu, ni kama kocha ambaye haijui kabisa timu yake.

Licha ya kumuacha nje ya kikosi Erasto, kocha huyo raia wa Nigeria ameendelea kung’ang’ania kumchezesha John Bocco katika eneo la pembeni wakati licha ya kukosa kasi, Bocco si mchezaji mzuri wa kutokea pembeni- Zaidi ni mkali akitokea kati na kukimbilia pembeni.

Stars inamuhitaji Zaidi Erasto kwa wakati huu kuliko timu hiyo inavyomuhitaji kwa sababu hii inaweza kuwa sehemu yake ya mwisho kuichezea timu ya Taifa kwa sababu amepanga kustaafu soka la ngazi ya Kimataifa.

Sambaza....