Alex Sanchez, amepata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo dhidi Southampton uliopigwa Jumamosi iliyopita, na Ole Gunnar Solskjaer anaamini atakosekana kwa wiki sita
Meneja wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kua Sanchez atakosekana kati ya wiki nne hadi sita. Sanchez alianza katika ushindi wa 3-2 dhidi Southampton mchezo uliopigwa Old Trafford, lakini alilazimika kutoka mapema kipindi cha pili kufuatia kugongwa mguu wake wa kulia na Jan Bednarek
Sanchez, raia wa Chile anaingia kwenye orodha kubwa ya majeruhi na anakua moja kati ya wachezaji 10 wa kikosi cha kwanza watakakosa mcheza wa Jumatano wa ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya 16 bora mkondo wa pili dhidi ya Paris Saint Germany, Paul Pogba anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo uliopita ambapo United ilipoteza kwa mabao 2-0 Old Trafford
Matatizo ya majeruhi kwenye kikosi cha United ina maana Solskjaer atakua na chaguo dogo, lakini kwa mara nyingine tena amewajumuisha wachezaji vijana Tahit Chong, Angel Gomez, Mason Greenwood, James Garner na mlinzi wa kushoto Brandon Williams ambao wote wamesafiri kuelekea Paris
United itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na shinikizo kidogo kutokana na matokeo ya mchezo kwanza, lakini Solskjaer amekanukuliwa akisema “Ikiwa hakunu anayekuamini hiyo ni nafasi ya kuonesha kile unachoweza kufanya”
Wachezaji hawatumiki kwa ajili kupoteza, na hatukua na furaha na matokeo ya kupoteza nyumbani” aliongeza kocha huyo