Nahodha wa timu ya Taifa Tanzania “Taifa Stars” na mshambuliaji wa Aston Villa amesema inaweza ikawa sawa ama sio sawa pia kwa wachezaji kukatwa mishahara kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona.
Kumekuwepo na pendekezo la wachezaji katika EPL kukatwa kwa asilimia 30 ya mishahara yao ili kuweza kusaidia mapambano ya ugonjwa wa Corona huku Barani Ulaya wakiwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.
Mbwana Samatta “Nadhani ni sawa na sio sawa pia kwa wachezaji kukatwa mishahara kwa kipindi hiki. Sio sawa kwasababu sio tu wachezaji wanaingiza kiasi kikubwa cha pesa, kuna makampuni mengine yanaingiza pesa nyingi tuu tena zaidi ya wachezaji wa mpira.
Mi nadhani ni vyema wangewaacha wachezaji wenyewe ndio waamue kuhusu kukatwa mishahara lakini isiwe kama shinikizo hivi. Wachezaji wa mpira ni watu wakarimu hivyo naamini wataamua wenyewe kukatwa mshahara kwa kipindi hiki.
Nadhani wachezaji ndo wamekua “target” kubwa kwasasa sio vibaya, ni vyema kila mwenye nafasi akachangia katika hili.”
Mbwana Samatta amesema hayo akiwa anaongea na katika kipindi cha michezo cha Azamtv.