Nahodha wa timu ya Taifa “Taifa Stars” na mshambuliaji wa Aston Villa Mbwana Samatta baada ya jana kufunga goli ametoa ya moyoni alipokua akiongea na mtandao wa klabu yake hiyo mpya.
Samatta alitumia dakika 69 kufunga goli lake la kwanza katika mchezo wa kwanza wa Epl akiwa na Aston Villa katika mchezo dhidi ya Bornemouth. Hata hivyo mchezo huo uliisha kwa Villa kupoteza kwa mabao mawili kwa moja.
Samatta “Ni sawa unapofunga goli kama mshambuliaji, lakini unapopoteza mchezo huwezi kuwa na furaha kwasababu kama timu tunatakiwa kushinda pamoja na kupoteza pamoja.”
Mpaka sasa Aston Villa imeshuka dimbani mara 25 huku pia ikiwa na alama 25 ikiwa nafasi ya 17, huku ikiwa juu kidogo ya mstari wa kushuka daraja.