Mshambuliaji wa Simba Pape Osmane Sakho ni miongoni mwa wachezaji walioitwa katika timu ya Taifa ya Senegal itakayoivaa Msumbiji katika michezo miwili yakufuzu Afcon.
Aliou Cise ametaja kikosi cha wachezaji 24 watakaoiunda timu ya Taifa ya Senegal ambacho kitaingia kambini hivi punde kujiandaa na michezo miwili itakayopigwa Machi 24 na kurudiana Machi 28.
Pape Osmane Sakho mshindi wa bao bora la Afrika mwaka jana amejumuishwa na washambuliani wengine wanaocheza Ulaya kama Sadio Mane [Bayern Munchen] Bamba Diengo [Lorient], Dia [Salernitana], Ndiaye [Sheffield United] na Diallo wa Strasbourg ya Ligue 1 Ufaransa.
Sakho amekua na kiwango cha kupanda na kushuka hivi karibuni akiwa na klabu yake ya Simba lakini amekua bado ni silaha muhimu kwa kocha Robertinho Oliveira na akitegemewa kuivusha klabu yake ya Simba kwenda robo fainali hapo kesho.
Baadhi ya wachezaji wengine wa Ulaya wanaocheza klabu kubwa na maarufu barani humo ambao wataungana na Sakho katika kikosi hicho ni pamoja na Gana Gueye, Khalidou Coulibaly, Pape Sarr na Keprin Diatta.