Mshambuliaji wa pembeni wa Simba Pape Osmane Sakho ameonekana kuwa lulu katika vilabu vya Afrika Kusini baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na Simba.
Kwa mujibu wa mtandao wa Kickoff Magazine kutoka Afrika Kusini vilabu vya Soweto Kazier Chiefs na Orlando Pirates vimeonyesha kuhitaji huduma ya winga huyo kutoka Senegal.
Ikiwa ana msimu mmoja tuu na Simba akijiunga nao akitokea Teungueth ya nchini kwao Senegal ameonekana kuwa moja ya nyota tishio kwa Wekundu hao wa Msimbazi haswa katika kampeni za Kombe la Shirikisho Afrika.
Sakho anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaosafiri na Simba kuelekea nchini Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano dhidi ya Orlando Pirates. Sakho alikuepo pia katika mchezo wa awali ambao Simba walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Licha ya kuanza taratibu katika kikosi cha Simba lakini sasa amenekana kuzoeana na wenzake na kua tishio kiasi cha kuendelea kuliziba vyema pengo la mtangulizi wake Luis Miquissone aliyejiunga na Al-Ahly.