Wapwa, nadhani hiii ndiyo iliyo maanishwa kwenye wimbo ‘halifichiki pembe la ngombe’
“Performance” ya Saidoo ukiiangalia tu unaiona kwa macho tangu siku ya kwanza pale ‘Lunyasini ‘ kaweka mipira 3 nyavuni dhidi ya Tanzania Prisons.
Siku ya mwisho wa msimu katia kamba 2 katikachezo dhidi ya Coastal Union katika dimba la Uhuru, mwanzo mzuri mwisho mzuri pia.
Nikajaribu kuangalia sajili nyingine za kipindi hicho cha dirisha dogo zile za kimataifa kama ya Ismail Sawadogo (akitokea Burkina Faso kwenda Simba) ,Momo Doumbia (akitokea Mali kwenda Yanga) na Yacuba Songne (akitoka Yanga kwenda Ihefu) Nelson Okwa akitoka Simba kwenda Ihefu na nyinginezo nyingi.
Lakini pia zile za ndani Rashid Juma aliyekwenda Ihefu akitokea Ruvu Shooting ,Hussein Abel Masalanga akitoka Prisons na kujiunga na KMC Fc, Yahaya Mbegu wa Geita aliyejiunga na Ihefu nk.
Hii ya Saido ndiyo bora bora zaidi na uthibitisho wa hili inaweza kuwa “mituzo” hiyooo na kwa kuipa uzito niitamke kama baadhi ya watu ‘Tunzo’.
Huyu mwamba ni “Professional” sana kwa kweli hata vitu alivyotupia siku hiyo inaweza kusadifu kutokana na tukio lenyewe lilivyohusu na yeye alivyotokelezea.
Maana yake kungekuwa na tuzo kwenye eneo ya “nominee” aliyenoga zaidi huwenda pia ingekwenda kwake pia mambo ya Paris France hayoo.
Saidoo Ntibazonkiza alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Geita Gold Fc. Msimu huu Saidoo amefunga mabao 17 na kutoa pasi 12 za mabao.