Ilikuwa ni “Super Performance” toka kwa Said Ndemla, alilalia upande ambapo game ilipoamkia na kujikuta yeye mwenyeji wa game.
Nakumbuka kabla ya mechi nilielezea Simba itakavyonufaika na uwezo wake wa kupiga pasi sahihi za mbali (long passes) hakika alizitendea haki sana kuwafanya “wing back” zote mbili Tshabalala na Kapombe kutakata sana kwa movement zao.
Lakini ili apige pasi hizo yeye anaupata mpira toka wapi? Hapa ndio ubora wake ulipo onekana kutafuta nafasi na kujiposition pale mpira unapokuwa upande wao ,hususani kwa mabeki. Anakwenda kutengeneza “triangle” zenye faida kwenye mashimo yote ya kulia na kushoto na akipokelea kushoto basi tarajia pasi ndefu kuelekea kulia na kama akipokelea kulia tarajia pasi ndefu upande wa kushoto.
“Turning up” zake kwa maana ya ufundi wa kugeuka, “acceleration speed” mara apatapo mpira kulikuwa na burudani ya aina yake, kwa kifupi alikuwa kwenye fomu ya juu kwa majukumu ya aliyopewa na hasa mfumo wa Simba wa jana 3-5-2.
Simba waliamua kuswitch mfumo wao ambao wamekuwa wakicheza siku zote Sina hakika kama Said Ndemla aliwahi kumuona Paul Scholes akicheza, kama alipata kumuona labda kuna vitu alicopy kwake, kwa kile nilichokiona kwake jana akili yangu ilihama na kudhani Scholes amerejea kucheza soka na kujikuta kaangukia Tanzania kwenye Club ya Simba.
Pamoja na yote najua alikuwa na nguvu za kutosha na ari kwa sababu hajacheza siku nyingi katika kikosi cha kwanza kwenye mechi za kimashindano yawezekana alitunza nguvu nyingi mwilini ndio maana alikuwa na wakati mzuri katika muda wote wa mchezo.
Naami nilianza kuiona performance hii kwenye mechi mbili tatu za kirafiki za hapa karibuni ambapo naamini ndipo alipolishawishi benchi la ufundi, naam sina shaka sasa amelishawishi upya benchi la ufundi chini ya Sven na Matola ambae anaujua uwezo halisi wa Said Ndemla.
Asante Said Hamis Ndemla “Daktari” kwa kutukumbusha Paul Scholes.