Kutokana na uchezaji wake, Mayele huenda akaelekea Afrika Kaskazini msimu huu wa usajili, baada ya kuripotiwa kuwavutia Zamalek, Pyramids FC, na Esperance ya Tunisia.
Haya ni kwa mujibu wa Pulsesports, ambayo ilifichua kuwa Mayele amekataa ofa kutoka kwa klabu yake ya kumuongezea kandarasi, jambo ambalo lingemfanya aongeze mshahara wake wa mwaka mara mbili.
Mkataba wa sasa wa Mayele unamalizika mwishoni mwa msimu huu, na mchezaji huyo ameelezea nia yake ya kutafuta fursa mpya nje ya nchi.
Wakati huohuo, kwa upande wa Zamalek, imefahamika kuwa “The Whites” hao wanajaribu kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kufuatia msimu mbaya unaoishuhudia timu hiyo kwa sasa ikishika nafasi ya nne kwenye jedwali la ligi.
Pyramids FC, kwa upande mwingine, imekuwa na msimu mzuri, na kujihakikishia nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa wa CAF msimu ujao kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, na watakuwa na hamu ya kusajili wachezaji wa aina ya Mayele.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amecheza mechi tano za kimataifa kwa akiwa na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akifunga bao moja dhidi ya Gabon mwezi uliopita.