Hivi karibuni shirika la takwimu za michezo duniani la CIES, lilifanya takwimu za wachezaji wenye thamani ya juu duniani huku mshambuliaji nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya 49
Kwa mujibu wa takwimu hiyo iliyotolewa Jumatano, anayeongoza orodha hiyo ni mshambuliaji wa Paris St- Germain ya ufaransa, mbrazil Neymar 25, huku Lionel Messi 30, wa Barcelona akishika nafasi ya pili
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ameorodheshwa kunako nafasi ya tatu, hapa unaweza kushangaa ni kwa nini thamani ya Ronaldo imekadiliwa kuwa $96.6 milioni
Nitajaribu kufafanua kwa nini watafiti wa CIES walifikia uamuzi huo ambao pengine unaweza kuwashangaaza wengi
Ronaldo sio kinda tena
Tathimini ya thamani ya mchezaji sokoni huzingatia mambo mengi, moja muhimu ni umri
Ronaldo anakaribia kugonga miaka 33
Ronaldo sio mzee wa kustaafu lakini anafikia ukingoni mwa maisha yake ya uchezaji, ukizingatia umri wa kawaida wa wachezaji kustaafu ni miaka 35, wachezaji wenye umri wa juu kimsingi huumia zaidi na wanapoumia huchukua muda mlefu kupona
Hili ni jambo ambalo klabu huzingatia zinapomnunia mchezaji
Kasi ya mchezaji kufunga
Lionel Messi ana miaka 30, na ndiye wa pili kwa thamani ikitajwa kuwa ni $242.8 milioni
Moja ya sababu za mchezaji huyo wa Argentina kuwa na thamani ya juu ni kutoshuka kwa kiwango chake, na muendelezo wa kasi ya ufungaji mabao, Messi amefunga mabao kumshinda Ronaldo msimu huu (20 na Ronaldo 16) na kusaidia ufungaji wa mengine (tisa dhidi ya matatu)
Messi kwenye ligi ufungaji wake haukushuka ukilinganisha na msimu uliopita, Ronaldo aliyefunga mabao 25 kwenye La Liga 2016/17 msimu huu amefunga mara nne pekee, huku Messi akikaribia kufunga bao lake la 20
Kujifunga kwenye klabu
Jambo lingine linalozingatiwa ukikadilia thamani ni jinsi mchezaji amejifunga kwenye klabu yake ya sasa, Ronaldo amedumu Real Madrid tangu 2009 akitokea Manchester United licha ya uvumi wa mara kwa mara kwamba anaweza kuhamia England na Ufaransa lakini amesalia Real Madrid. Hii imeathili thamani yake sokoni
Matokeo ya timu
Ni mwezi Mei tu, ambapo Real Madrid walishinda La Liga na kombe la ligi ya mabingwa Ulaya kwa pamoja, na kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wa Ulaya katika rono karne
Ligi ya klabu bingwa Ulaya kwa sasa, Real Madrid walifika hatua ya mtoano kwa urahisi licha ya kupitwa na Tottenham Hotspur kwenye kundi na walishinda mechi nyingi Ulaya hatua ya makundi msimu uliopita
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Ronaldo na Real hawajafana msimu huu wa La Liga, Real Madrid msimu huu wametatizika La Liga baada ya mechi 18, wamo nafasi ya 4, alama 16 nyuma ya vinara Barcelona
Uchezaji wa klabu pia huchangia thamani ya mchezaji. Msimu huu Real Madrid wamekuwa wakipata wastani chini ya alama mbili kwa mechi La Liga
Lakini hata hivyo sina maana kwamba klabu zinaweza kutarajia kumnunua Ronaldo kwa bei ya kutupa
Mreno huyo analipwa mshahara wa $58 milioni kwa mwaka jana
Na bado amesalia miaka mitatu mkataba wake na Real Madrid
Baadhi ya nyota waliomo kwenye orodha hiyo ni
Kyalan Mbappe 19, ameshika nafasi ya nne akiwa na thamani ya $231.2
5.Paulo Dybala mwenye umri wa miaka 24, $209.7
6. Delle Alli mwenye umri wa miaka 21, $205.7
7. Kelvin De Bruyne 26, $201.5
8. Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 24, $197.9
9. Antoine Griezmann mwenye umri wa miaka 26 $180.4
10. Paul Pogba mwenye umri wa miaka 24 $177.1