Sambaza....

Tayari Simba walishavunja ndoa yao na Patrick Aussems , ndoa ambayo imedumu kwa kipindi cha msimu mmoja na robo. Ndoa ambayo ilikuwa na matunda kwa Simba kuchukua kombe la ligi kuu Tanzania pamoja na kombe la ngao ya jamii, bila kusahau kuifikisha Simba hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika, lakini amefukuzwa. Hizi ni sababu tatu ambazo zinaelezea kwanini


Klabu Bingwa Makundi

PosTimuPWDLGDPts
16312810
26303-79
36222-38

MAFANIKIO NDANI YA SIMBA

Kwenye kipindi chake ameipa mafanikio makubwa Simba kuanzia namna ambavyo timu ilivyokuwa ikicheza. Ilikuwa inacheza mpira wa kuvutia, mpira ambao Siku nyingi Simba hawajafanikiwa kucheza. Pamoja na aina ya mchezo ambao walikuwa wanacheza, Patrick Aussems alifanikiwa kuipa Simba kombe la ligi kuu ya Tanzania bara , kombe ambalo mpaka anaondoka alikuwa anaongoza ligi hivo alikuwa na uhakika wa kuendelea kulitetea.

KIKOSI KIPYA

Ukitazama wachezaji nyota ambao walichangia mafanikio ya Simba kwa kiasi kikubwa msimu jana waliondoka na kukawepo na ongezeko kubwa la wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Simba. Wachezaji kama James Kotei, Emmanuel Okwi waliondoka Simba. John Bocco alikumbwa na majeraha muda mrefu huku Chama akishuka kiwango kwa kiwango kikubwa.

Hawa ndiyo walikuwa chachu ya mafanikio kwa Simba msimu jana lakini msimu huu hawakuwa na mchango mkubwa sana. Ingizo la wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Simba ilichukua muda pia kuleta muunganiko mzuri. Patrick Aussems alikuwa ndiyo anaanza kuitengeneza timu.


PosTimuPWDLGDPts
13829636293

REKODI NZURI YA PATRICK AUSSEMS

Patrick Aussems wakati akiwa Simba ameiongoza Simba michezo 50, akashinda michezo 36 akatoka sare michezo 5 na kushinda michezo 15 huku akiwa na asilimia 72% za ushindi. Hii ni rekodi nzuri kwa kocha na msimu huu amefanikiwa kuipatia Simba alama 25 akiongoza ligi.

Sambaza....