Mlinda mlango wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Edwin Van De Sar anashikilia rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu goli katika michezo ya Ligi Kuu ya England EPL.
Edwin alicheza dakika 1311 bila kuruhusu goli langoni mwake akiwa na United katika msimu wa 2008/2009, ikijumuisha michezo 14 mfululizo. Rekodi hii inasimama mpaka leo na ikiwa ni miongoni mwa rekodi ngumu zaidi kuzivunja na walinda mlango wasasa.