Sambaza....

Klabu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imethibitisha kuinasa saini ya kiungo Mshambuliaji kutoka Yanga SC, Emmanuel Martin katika dirisha dogo la usajili linalotazamiwa kufungwa usiku wa kesho.

Taarifa za kusajiliwa kwa mchezaji huyo ambaye alikuwa akiicheze Yanga imetolewa na Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire ambaye amesena wameingia mkataba wa miezi sita na wings huyo.

“Klabu ya soka ya Ruvu Shooting imeingia mkataba wa miezi sita na mchezaji Emmanuel Martin Joseph, mchezaji huru baada ya mkataba wake na Klabu ya Yanga kumalizika Disemba13, 2018……Martin amesaini mkataba huo kuitumikia Ruvu Shooting leo, December 14, 2018 mbele ya Katibu msaidizi wa Ruvu Shooting, Issa Mikwele,” taarifa hiyo imeeleza.

Martin ambaye ni mahiri katika nafasi ya ushambuliaji akitokea pembe ya kushoto na kulia (7 na 11), pia namba 10, amesajiliwa na Ruvu Shooting kuongeza nguvu katika safu hiyo baada ya kocha mkuu Abdulmutiki Haji Kiduu na benchi lote la ufundi kuona uwepo wa uhitaji huo na kwamba Martin ni mchezaji atakayeweza kusaidia timu katika nafasi hiyo.

“Kikosi cha Ruvu Shooting kimekamilika, kazi sasa ni kumpapasa squad kila atakayekatiza mbele ya kikosi hiki hatari, Jumapili kikianza makeke yake dhidi ya Yanga, uwanja wa Taifa, Dar es salaam,” Taarifa ya Masau Bwire imeeleza.

Kabla ya kusajiliwa na Ruvu Shooting, Martin alikuwa akiichezea Yanga SC, timu nyingine alizowahi kuzichezea ni pamoja na Ukwamani FC, JKT Mlale na JKU ya Zanzibar .

Sambaza....