Chelsea katika dirisha hili dogo la usajili wamefanikiwa kumchukua kiungo Ross Barkley kutoka katika timu ya Everton.
Wana idadi kubwa ya viungo wa kati kama Kante, Bakayoko, Fabregas, Danny Drink-Water.
Viungo wote hawa kuna kitu Chelsea wanakosa katika eneo hili la kiungo ?
Hebu tujaribu kuwatazama viungo waliopo kwa sasa.
Kante : Kazi kubwa ya Kante ni kuilinda safu ya ulinzi ya Chelsea na kuanzisha mashambulizi.
Kazi hii Kante amekuwa akiifanya kwa kiwango kikubwa sana.
Fabregas: Kazi kubwa ni kutengeneza nafasi za magoli kutokea katikati ya uwanja, hana kasi ya kukimbia kutoka katikati kwenda mbele ila ana uwezo wa kupiga pasi ndefu na za mwisho akitokea katikati ya uwanja.
Kazi hii anayoifanya Fabregas haipishani na kazi ambayo imemleta Danny Drink-Water na ndiyo maana aliletwa kwa madhumini ya yeye kuja kuwa mbadala wa Fabregas.
Kante na Fabregas wanatimiza vizuri majukumu yao, ila kinachokosekana ni kiungo ambaye anakimbia kuanzia nyuma mpaka mbele ( kiungo atakayesaidia eneo la ulinzi na eneo la ushambuliaji).
Bakayoko ndiye ambaye ameletwa kwa ajili ya kufanya hiyo kazi lakini anakosa kitu kimoja, nacho ni ubunifu wa kutengeneza nafasi za kufunga na uwezo wa kufunga.
Hiki ndicho kinachokosekana na hapa ndipo mahali ambapo Ross Barkley atakapokuwa na msaada mkubwa.
Je anawezaje kucheza katika mifumo ya Conte?
Conte amekuwa akitumia 3-4-3 na 3-5-2.
Nyuma akiwa na mabeki watatu ambao ni Cahil, Azplicueata na Andreas Christensen.
Ili kumfanya Ross Barkely aingie katikati basi itamlazimu acheze na Kante, Fabregas/Drink-Water na yeye. Huku kwenye wingback ya kushoto akicheza Marcus Alonso na Wingback ya kulia akicheza Victor Mosess.
Na mbele wanacheza Hazard, Morata na Pedro
Kwenye mfumo 3-4-3 pia, Ross Barkley anaweza akacheza pembeni eneo la Willian/Pedro.
Hivo mabeki wanabaki wale wale watatu ( Cahill, Azplicueta na Christensen).
Eneo la katikati wakacheza Kante, Fabregas/Drink-Water. Huku wingsback ya kushoto akacheza Marcus Alonso na Wingback ya kushulia akacheza Victor Mosess.
Na mbele akacheza Hazard ,Morata na Yeye mwenyewe Ross Barkley.
Pia na kwenye huu mfumo wa 3-4-3 pia Ross
Yani mabeki wanabaki walewale watatu niliowataja hapo juu, viungo wa kati anakaa Kante na Ross Barkley. Mbele waweza kutumia njia mbili , njia ya kwanza ni ya kumfanya Fabregas acheze, hivi unampeleka nyuma ya mshambuliaji wa mwisho na umbo linakuwa 3-4-1-2 huku Hazard akicheza kama mshambuliaji huru na Morata kubaki kama mshambuliaji wa mwisho. Huku wingbacks wakibaki wale wale Alonso na Mosess upande wa kushoto na kulia.
Umbo la pili ni umbo ambalo litamuondoa Fabregas na kuwaweka Willian au Pedro kule mbele (3-4-3). Mabeki wanabaki wale wale watatu. Wingback wanabaki wale wale. Katikati anabaki Kante na Ross Barkley, mbele ndiyo wanakuwa Hazard , Morata na Pedro/Willian.
Upi ni ubora wa Ross Barkley?
Kukaa na mpira, hii inaweza ikaonekana kama hasara ila ni faida sana.
Mchezaji anapokaa na mpira husaidia wachezaji wenzake watafute sehemu zenye uwazi ili wawe huru kupokea mpira.
Uwezo wa Barkely kukaa na mpira kutakuwa na msaada mkubwa kwa wachezaji wa Chelsea kuwa na nafasi ya kutafuta sehemu zilizo wazi ili wapokee mipira.
Kuunganisha na kuanzisha mashambulizi ni faida nyingine ya Ross Barkley.
Huwa anatabia ya kushuka chini kuchukua mpira nyuma na kusaidia kuunganisha timu kwa kuanzisha mashambulizi.
Mtu wa aina hii alikuwa anakosekana Chelsea ndiyo maana kuna kipindi Hazard huwa anashuka kuchukua mipira chini, uwepo wa Ross Barkely kutamfanya Hazard asiwe anashuka mara kwa mara chini.
Ross Barkely pia anauwezo wa kutengeneza nafasi kwa ubunifu mkubwa. Bakayoko amekuwa siyo mtu mbunifu kwenye kutengeneza nafasi.
Kuna kitu ambacho kinambeba sana Ross Barkley, nacho ni uwezo wake wa kufunga ndani na nje ya box .
Anauwezo wa kufunga kwa mashuti akiwa nje ya box,na hiki kinambeba sana.
Kwa hiyo, baada ya Bakayoko kukosa ubunifu mkubwa katika eneo la mwisho , Ross Barkley atakuja kuongeza ubunifu ambao ulikuwa unakosekana wakati wa Bakayoko