Sambaza....

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Robert Oliveira amesema hana mashaka na morali ya wachezaji wake kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Vipers.

Robertinho amesema wamepata muda wakutosha wakufanya mazoezi na wachezaji wake wamebadilika na anaamini katika Mungu kuelekea mchezo huo.

 

Robert Oliveira “Mimi ni mtu chanya siku zote, nina muamini Mungu, nawaamini wachezaji wangu, nina miezi mitatu tangu niwe hapa lakini tumeanza kubadilika kiuchezaji.”

Pia kocha huo ameongeza wapinzani wake anawajua kwani amewasoma vyema na anajua jinsi ya kuwadhibiti Waganda hao.

Robertinho Oliveira

“Vipers ni timu nzuri, inacheza soka la kushambulia kwa kushtukiza, tumefanya maandalizi ya kuwadhibiti ili tupate ushindi. Ninaamini hatua kwa hatua tunaweza kuvuka na kuingia robo fainali,” amesema Robertinho.

Simba itashuka Dimbani leo saa moja jioni kuvaana na Vipers katika mchezo wa nne wa Kundi C wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sambaza....