Real Madrid wanaizamisha Liverpool katika mchezo wa fainali nchini Ukraine katika jiji la Kyiev kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Karim Benzema na Gareth Balle wanaifungia Madrid huku Saido Mane akifunga bao la Liverpool.
Baada ya ushindi huo wa Madrid rekodi mbalimbali zimewekwa za binafsi na timu. Rekodi zilizowekwa hizi hapa:
Real Madrid ndio timu iliyochukua kombe la klabu bingwa ulaya mara nyingi zaidi kuliko klabu yoyote Ulaya. Imechukua mara 13 mpaka sasa. Ikifwatiwa na AC Milan (7) Barcelona, Bayern na Liverpool (5)
Real Madrid ndio timu pekee iliyochukua kombe hilo mara tatu mfululizo. Imeweza kufanya hivyo mwaka 2018, 2017 na 2016, huku wakizifunga Liverpool, Juventus na Athletico Madrid kwenye fainali.
Zinedine Zidane ndie kocha pekee aliyeweza kushinda kombe hilo mara tatu mfululizo pia na Sergio Ramos akiwa kama nahodha amewaza kulichukua mara tatu mfululizo (2016, 2017, 2018).
Zinedine Zidane akiwa na Real Madrid anaungana na Carlo Ancheloti akiwa na timu tofauti kuwa makocha waliobeba kombe la ligi ya mabingwa ulaya mara tatu.
Mreno Christiano Ronaldo ameshinda kombe la mabingwa ulaya mara 5, mwaka 2008 akiwa na Man United mwaka 2014, 2016, 2017 na 2018 akiwa na Real Madrid. Hivyo kumfanya kuwa sawa kwa mataji na vilabu vikubwa duniani kama Barcelona Liverpool na Bayern Munich walioshinda kombe hilo mara 5 pia.
Christiano Ronaldo ameshinda fainali nyingi za ligi ya mabingwa ulaya kuliko mchezaji yoyote (mara 5). Akifwatiwa na Clarence Seerdolf na Andres Iniesta akiwa na Barcelona walioshinda mara nne.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amepoteza fainali 6 tangu aanze kufundisha soka akiwa Liverpool na Borusia Dortmund ya Ujerumani, amepoteza;
Fainali mbili za ligi ya mabingwa ulaya 2018 & 2013.
Fainali moja ya Europa league 2016.
Fainali mbili za Kombe la Ujerumani 2015 & 2014.
Fainali moja ya kombe la ligi 2016.