Baada ya kushuhudia vilabu vya Barcelona na Manchester city, vikitupwa nje ya michuano Uefa Champions League leo hii tutashuhudia Bayern Munich wakikaribisha Sevilla, lakini pia Real Madrid wataikaribisha Juventus ya Italia
Juventus hawana rekodi ya kuridhisha wanapoingia kunako dimba la Santiago Bernabeu, katika michezo 8 waliyocheza kunako uwanja huu wameshinda mara mbili tu na kwenda sare mmoja huku michezo 5 wakipokea vichapo
Huu ni mchezo wa 22 unazikutanisha vilabu hivi na katika michezo 21 waliyokutana Real Madrid wamefanikiwa kushinda michezo 10, Juventus wakishinda mara 9 huku michezo miwili wakienda sare
Katika michezo 32, ya hatua ya mtoano ambayo Real Madrid walianzia ugenini na kushinda, ni mara moja pekee ndio walishindwa kufudhu ikiwa ni msimu wa mwaka 1994/95 ambapo waliifunga 3-2 Odense Boldklub ugenini kabla kukubali kichapo cha 2-0 nyumbani
Christiano Ronaldo ataendelea kuwa tishio kwa safu ya ulinzi ya Juventus, kutokana na rekodi zake ambapo katika michezo yote 6 aliyokutana na Juventus amefanikiwa kufunga mabao 9