Baada ya jana Juventus kurudisha matumaini yao ya kubeba kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996, Cristiano Ronaldo aliibuka shujaa tena.
Alionesha thamani yake, alionesha kwanini alistahili kuwashawishi Juventus kutoa Euro milioni 112 kwa ajili ya kumleta katika uwanja wa Allianz Stadium.
Na jana ameonesha dhahiri kazi ambayo ilimleta pale Turin baada ya kufunga hattrick na kuifanya Juventus ifuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Je rekodi ipi ambazo Cristiano Ronaldo aliziweka baada ya kufunga hat trick dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa jana?
1: Màgoli matatu aliyoyafunga jana yamemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 125 katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya, na ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli mengi katika michuano hii ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
2: Hattrick ya jana imemfanya afikishe Hattrick yake ya nane katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa analinga na Linonel Messi ambaye na yeye ana hattrick nane katika michuano hii ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
3: Hattrick aliyoifunga jana dhidi ya Atletico Madrid imemfanya kuwa mchezaji ambaye ameifunga Atletico Madrid hattricks nne, na Timu ambayo anaongoza kuifunga hattrick nyingi ni Sevilla. Kwa hiyo kwa hattrick ya jana , imemfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kuifunga hattrick Timu moja kwa mara mbili.