Baada ya kupitia nyakati ngumu , klabu ya Yanga kwa sasa iko kwenye nyakati za Neema. Yanga ilikuwa imeshindwa kulipa mishahara kwa wachezaji wake mpaka kufikia wakati wa baadhi ya wachezaji kuandika barua za kuomba kuvunja mkataba kutokana na kutolipwa.
Kupitia kwa Afisa Mhamasishaji wa Yanga , Antonio Nugaz kwa sasa matatizo hayo kwa sasa hayapo tena. “Kupitia wadhamini wetu brand Chapa GSM, Taifa Gas na Sportspesa kwa sasa hakuna hayo matatizo “.
“Hutosikia tena wachezaji wakidai mishahara , mashabiki wa Yanga wanatakiwa kunywa Gahawa bila wasiwasi kwa sababu kwa sasa hakuna njaa tena kama awali”.
Kuhusu Mrisho Ngassa Afisa huyo Mhamasishaji amedai kuwa kwa sasa wameshamalizana na Mrisho Ngassa ndiyo maana alikuwa wa kwanza kufika Mbeya.
“Mrisho Ngassa kwa sasa anatabasamu tu, tushamalizana naye ndiyo maana alikuwa wa kwanza kufika mjini Mbeya kwa ajili ya pambano kati ya Mbaya City na Yanga”-alimalizia Afisa Mhamasishaji huyo wa Yanga