Baada ya kuachana na Yanga aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo George Lwandamina leo hii katangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Zesco United.
Mtendaji mkuu wa klabu hiyo ( Zesco United) Richard Mulenga amemtangaza George Lwandamina kuwa kocha mkuu sambamba na Alfred Lupiya kuwa kocha wa kwanza msaidizi huku Emmanuel Siwale atabaki kuwa kocha kocha wa pili msaidizi.
Hii ni mara ya pili kwa George Lwandamina kuifundisha Zesco United baada ya kuachana nayo mwaka 2016 ambapo alifanikiwa kuipa mafanikio makubwa sana ikiwepo kuifikisha hatua ya nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.
Alifanikiwa kuipa makombe yafuatayo pia. Zambian Super League mara mbili ( 2014 na 2015). Akachukua Barclays Cup mwaka 2014.
George Lwandamina ambaye aliwahi kuwa kocha bora wa Zambia mwaka 2014 na 2015 alianza kazi yake ya ukocha kwenye timu ya Mufulira Wanderes kama kocha msaidizi mwaka 1995 baada ya hapo alienda kusoma Ujerumani na aliporudi Zambia mwaka 1997 alifanikiwa kuipeleka Mufulira Wanderes robo fainali ya mashindano ya vilabu ya CAF.
Amewahi kuzifundisha pia Buffaloes , Kabwe Worriors na vilabu vingine nchini Zambia.
Na amewahi kuwa kocha msaidizi wa Zambia vipindi tofauti. Kipindi ambacho Kalusha akiwa kocha mkuu na kipindi ambacho Patrick Phiri akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia