Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la soka nchini (TFF) na viongozi wa kiserikali umeondoka mchana wa leo kuelekea nchini Algeria.
Wakiondoka na ndege ya Shirika la ndege la Tanzania “Air Tanzania” msafara huo umeonekana ukiwa na hamu kubwa ya kurudi na kombe la ubingwa wa Shirikisho kutokana na morali kubwa waliyonayo wachezaji wa Yanga.
Rais wa TFF Wallace Karia akiwa ni miongoni mwa watu waliopo kwenye msafara huo wa Yanga amesema “Hili kwa sasa sio jambo la Yanga bali ni kitaifa, kwahiyo tupo pamoja kuhakikisha tuma chukua ubingwa na nimewasikia wachezaji wakiwa wanazungumza wanahitaji ushindi.”
Nae mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kinara wa mabao wa michuano hiyo ya Shirikuasho Afrika amewataka Watanzania na mashabiki wa Yanga kuwaombea kuelekea mchezo huo.
Fiston Mayele “Mashabiki wa Yanga watusapoti na watuombee kwa Mungu ili mambo yaende vyema.”
Yanga baada yakupoteza kwa mabao mawili kwa moja wakiwa uwanja wa nyumbani sasa wanahitaji ushindi wa mabao mawili kwa bila ili kuweza kupindua meza mbele ya USM Algier.
Mchezo huo utacheza June 3 Jumamosi saa nne usiku kwa saa za Tanzania katika Dimba la Stadium de 5 Juillet Algiers.