Azam Fc wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Azamsports Federation cup na kufanikiwa kutinga fainali.
Azam wamefanikiwa kuwatoa Simba lakini kitu cha kuvutia zaidi ni historia ya Prince Dube na Simba katika upande wa mabao haswa katika michezo ya msimu huu ambapo Dube amefanikiwa kuwafunga katika michezo yote waliyokutana.
Katika mchezo huo Azam Fc walikua wakwanza kupata bao kupitia kwa mlinzi wake wa pembeni Lusajo Mwaiekenda aliyemalizia mpira uliookolewa vibaya na Ally Salim uliotokana na mpira wa adhabu katika dakika ya 28 ya mchezo.
Simba walitulia na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 28 kupitia kwa kiungo wake Sadio Kanoute “Putin” akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Said Ntibazonkiza na hivyo kwenda mapumziko wakiwa sare.
Kipindi chapili alitoka Idris Mbombo na kumpisha Prince Dube ambae hakufanya ajizi katika dakika ya 75 aliifungia timu yake ya Azan bao la pili na la ushindi na kuendelea na rekodi yake yakuinyanyasa Simba kila wanapokutakana.
Katika msimu huu pekee Azam na Simba wamekutana mara tatu, mara mbili katika Ligi ambapo Azam alishinda mchezo wa kwanza na sare katika mchezo wapili na huu wa FA ambao Simba imetolewa. Na katika michezi yote hiyo mitatu Prince Dube amefunga hivyo anakua na mabao matatu dhidi ya Simba
Kwa matokeo hayo sasa Azam Fc wameshatangulia fainali na wanamngoja mshindi kati ya Yanga au Singida Big Stars katika nusu fainali ya pili.
Simba sasa baada ya kutewa na Azam ni rasmi hawajachukua kikombe chochote msimu huu kutoka mashindano ya mtoano kwani walilikosa kombe la Mapinduzi pia wakatolewa Ligi ya Mabingwa nasasa wameondoshwa katika FA.