Kocha mkubwa na mwenye mafanikio kabisa katika bara la Afrika Pitson Mosimane amekubali uwezo wa kocha wa Yanga Nasraddine Nabi na kusema anafaa kutimkia Afrika Kusini na kuinoa Kazier Chiefs.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha nchini Afrika Kusini Pitso alipouliza kama Nabi anafaa kuifundisha Kaizer Chiefs Pitso alisema “Ni mtu mzuri, kocha mzuri,” na kuongeza “Ameshinda mataji matatu mara mbili, sio watu wengi wameshinda mataji mara tatu mara mbili. Nadhani niliipata mara mbili lakini kwa miaka tofauti, lakini (Nabi) aliipata miaka miwili mfululizo.”
Lakini pia Pitso alimuonya Nabi na kumwambia kocha huyo Mtunisia ushindani wa ligi ya PLS ni mkubwa zaidi ya ligi ya Tanzania.
“Soka la Afrika Kusini si sawa na Tanzania. Soka la Tanzania ni Yanga, Simba, Azam na nyinginezo bila kumdharau mtu yeyote.”
Kocha Nabi anajua stresi, anajua presha za kufanikiwa. Anajua aina hiyo ya stresi kwa hiyo angeweza kushughulikia presha na stresi vizuri. Na amethibitisha kuwa ni mzuri katika hilo, aliifikisha Yanga katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.”
Amakhosi walikuwa na msimu mbaya ambapo katila msimu wa 2022/23. Chiefs walimaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi na kukosa kushiriki mashindano ya CAF ya vilabu.
Walicheza michezo 13 kwenye ligi, sare tano na kupoteza mara 12 katika mechi 30 huku wakijikusanyia pointi 44. Huku Chiefs ikionekana kutaka kufanya mabadiliko ya timu ya ufundi, ni wazi kocha wa sasa Arthur Zwane ataonyeshwa mlango wa kutokea.
Tayari vyombo mbalimbali vya Afrika Kusini vinaripoti Nasraddine Nabi yupo katika hatua za mwisho kutambulishwa na wababe hao kutoka Soweto.