Kocha wa Manchester city Pep Guardiola, amekataa kumlaumu mshambuliaji wake Raheem Sterling baada kikosi chake kushindwa kupata ushindi dhidi Bunley huku mshambuliaji huyo akikosa nafasi ya pekee.
Ikiwa mbele kwa bao 1-0 na dakika 18, zikisalia ili mchezo huo kumalizika, Sterling alishindwa kufunga akiwa ndani ya sita baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Kyle Walker.
Tukio ambalo lilipelekea kuzomewa na mashabiki wa City, huku mchezaji huyo akitolewa nje mara moja kabla ya Johann Berg Gudmundsson hajaisawazishia Burnley ikiwa zimebaki dakika 10, mchezo kumalizika
Lakini kocha wa City Pep Guardiola amesisitiza kuwa hakumtoa Sterling kwa sababu ya kukosa nafasi hiyo ya wazi
Wakati hayo yakiendelea huko, mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez alifunga bao lake la kwanza akiitumikia timu hiyo huku ikipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Huddersfield town na kuionesha mlango wa kutelemka daraja
Mshambuliaji Romero Lukaku Bolingoli raia wa Ubeligiji aliipatia United bao la uongozi kunako dakika ya 54, baada ya kupokea mpira wa klosi kutoka kwa Juan Mata
Sanchez, alifunga bao la pili kwa mpira wa kurudi baada ya mkwaju wake wa penati kupanguliwa na kipa wa Huddersfield, na kufanya awe amefunga goli lake la kwanza baada ya mechi tatu akiwa na jezi ya Manchester united.
Beki wa Huddersfield Michael Hefele alimuangusha Sanchez ndani ya eneo la hatari ndipo mwamuzi Stuart Attwell akaamuru penati hiyo.