Sambaza....

Kukiwa na taarifa ya aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba , Patrick Aussems kuchukuliwa na klabu ya Yanga kuwa kocha mkuu kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera , Yanga wamedai Patrick Aussems ndiye aliyejipendekeza kwao.

Akizungumza na kituo cha Habari cha Wasafi FM , Afisa Habari Wa Yanga , Hassan Bumbuli amedai kuwa kocha huyo ndiye aliyeifuata Yanga kutaka kuifundisha.

“Baada ya kuondoka kwa Mwinyi Zahera makocha wengi wameitaka nafasi yake , moja ya makocha ambao walituma maombi ya kuifundisha timu ya Yanga ni huyu kocha mpya wa Simba , Baada ya sisi kumkataa akaona aende Simba kuomba nafasi ya kufundisha”

“Pia aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Simba , Patrick Aussems ni moja ya watu ambao walituma maombi ya kuifundisha Yanga , na bado tunamtazama kwa sasa na taarifa zitawajia punde ” alimalizia Afisa Habari huyo Wa Yanga. Yanga kwa sasa iko chini ya kocha wa muda Charles Boniface Mkwasa.

 

Sambaza....