Sambaza....

Kila wiki mtandao wetu utakuwa unaangalia nani shabiki wake maarufu katika kuchangia maoni ndani ya mtandao huu kwenye makala, habari, ratiba au popote ndani ya mtandao wetu. Ikiwamo na sehemu ya ‘#KandandaChat ya leo‘ ambayo itakuwa inaangazia mijadala mbalimbali inayohusiana na mpira wa miguu.

Nini unatakiwa kufanya?

Changia maoni kadri uwezavyo yasiyopungua ishirini katika mtandao wetu ukitumia akaunti yako ya Facebook ukiambatanisha na hashtag ya #BandoKa.

Utashindaje?

Mtandao wetu utaangalia ni shabiki wetu gani amechangia zaidi katika mtandao kwa wiki husika, huyo atakuwa ni mshindi wetu na atajipatia bando nono la wiki katika namba ya simu ya mtandao anaoutumia.
Nafasi ya kushinda zipo wazi, hakikisha unachangia vizuri kwa lugha yenye nidhamu, kwakuwa mtandao wetu unatembelewa na watu wa rika zote.

Washindi wangapi kwa wiki?

Kwa sasa tunaanza na washindi wawili tu kwa wiki.

Upo tayari ku “#BandoKa na Kandanda”? Anza sasa….


Sambaza....