Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Parimatch Tanzania leo imetimiza adhima yao ya kusaidia timu zenye uhitaji muhimu na ambazo ziliweza kushiriki katika kinyang’anyiro cha shindano la Amsha ndoto ambalo linaendeshwa kisasa mtandaoni kwa kuwapatia jezi, mipira pamoja na bibs za kufanyia mazoezi.
Shindano hilo ambalo lilizinduliwa rasmi mnamo Julai 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana na kuzitaja timu hizi kuwa ni Lifofo fc inayotokea Kawe, Bonyokwa fc iliyopo Tabata Segerea, Tambaza ya Kariakoo pamoja na Ilala United iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha, Maligana amesema kuwa, Parimatch imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii na kwamba Kampeni ya Amsha ndoto ni miongoni mwa sehemu ya kurudisha kupitia eneo la michezo.
“Tunafahamu michezo ni nguzo muhimu za burudani na afya hususani kwa vijana lakini pia kwa uendelevu wake, michezo ni ajira pia na ndio maana tukaamua kujikita katika timu ambazo hazipo katika daraja lolote zenye ndoto ili kusudi waweze kujiajiri kupitia michezo. Sisi kama Parimatch kwa uwezo tuliokuwa nao tutaweza kufanya kila liwezekanalo ili kuamsha ndoto za vijana zitimie na huu ni mwanzo tu lakini tutakapoona wadau wengine wa michezo wanaungana nasi katika hili baasi hii Amsha Ndoto itakuja kuwa ni kitu kikubwa sana”, amesema Maligana.
Pamoja na hayo, Maligana amewasisitizia vijana na wamiliki wa timu mbalimbali kuendelea kuchangamkia fursa kupitia tovuti ya amshandoto ili kusudi wapate kufikiwa kwa uwepesi.