Katika kutambua mchango wa waandishi wa Habari za michezo, idara ya habari na mawasiliano ya Pamba FC imekuja na tukio kubwa la Pamba Media Day ambapo litawakutanisha wanahabari wote wa michezo katika eneo moja na kuwaandalia “WORKSHOP” kwaajili ya kuongeza ujuzi ili kuwezeaha ufanisi wa kazi zao.
“WORKSHOP” hiyo itaendeshwa na Karim Boimanda Afisa Habari wa Bodi ya Ligi(TPLB) katika hoteli ya Mwanza Hoteli majira ya saa 3:00 Asubuhi.
Mbali na Hilo Pamba Fc limeandaa Burudani ya Mchezo wa mpira wa miguu ambapo Wafanyakazi wa Pamba FC(Pamba Staff) watacheza Dhidi ya waandishi wa Habari za michezo mkoa wa Mwanza majira ya Saa 9:00 Alasiri katika uwanja wa Nyamagana.
Matukio Yote Yatafanyika Jumamosi ya January 7 Mwaka huu. “Pamba Media Day” imelenga kumthamini Mwandishi wa Habari za Michezo.