Baada ya kutolewa na TP Mazembe katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Africa Simba ilikutana na ratiba ngumu ya viporo ambapo wanatakiwa kucheza mchezo kila baada ya masaa 48 au 72.
Simba ilianza kula viporo kwa timu za kanda ya ziwa huku wakiacha rekodi za kipekee. Timu walizotakiwa kucheza nazo katika ukanda huo ni Kagera Sugar, Allince School, Biashara na KMC iliyohamia katika dimba la CCM Kirumba baada ya kupisha Afcon jijini Dar es salaam.
Mpaka sasa Simba imecheza michezo mitatu huku wakishinda miwili dhidi ya KMC na Allince fc huku ikipoteza mbele ya Kagera kwa mabao mawili kwa moja.
Emmanuel Okwi
Simba baada ya kucheza michezo mitatu mpaka sasa Kanda ya Ziwa Emmanuel Okwi amefanikiwa kufunga mabao matatu (vs Kagera Sugar, vs Allince fc, vs KMC).
Kabla ya Okwi kufunga katika mchezo wa Kagera alikua ana mabao 7 lakini baada ya kucheza michezo mitatu kanda ya ziwa sasa amefikisha mabao 10.
Aishi Manula
Kipa namba moja wa Timu ya Taifa na Simba amekua na wakati mmbaya akiwa kanda ya ziwa baada ya kutunguliwa vilivyo.
Katika michezo mitatu aliyokaa langoni Manula amefungwa mabao matatu pia.
Magoli mawili vs Kagera na goli moja dhidi ya KMC. Huku akipata cleansheet mchezo mmoja dhidi ya Allince fc.
Simba sasa imebakisha mchezo mmoja katika ukanda huo watakaoucheza kesho dhidi ya Biashara United ya Mara.