Kiungo wa zamani wa Chelsea Obi Mikel ameonyesha nia ya yeye kucheza barani Afrika huku akionyesha uwezekano wa kuelekea katika katika Ligi Kuu nchini Misri.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria “Super Eagles” ameonyesha lolote linaweza kutokea katika maisha yake ya soka na kutanabaisha bado ana nguvu na hamu ya kuendelea kucheza soka.
Obi Mikel “Kucheza kwenye Ligi Kuu ya Misri? Kwa nini isiwe hivyo?, Mimi ni mchezaji wa mpira wa miguu na kila kitu kinawezekana, sijawahi kukataa chochote.
“Lengo langu ni kuendelea kucheza mpira wa miguu, na natumai nitapata fursa, sijakataa ofa yoyote iliyotolewa kwangu, lakini mpaka nione ofa yenyewe kama ni nzuri ndipo nitakapofanya uamuzi sahihi.” Imeripotiwa na Kingfut
Mikel aliondoka Chelsea baada ya kukaa klabuni hapo misimu zaidi ya 10. Ambako alifaninikiwa kushuka dimbani mara 374 na kushinda mataji nane ya ligi ya nyumbani Uingereza na mataji mawili ya Ulaya.
Baadae alirudi kwenye soka la Uingereza kwa mkataba wa muda mfupi katika klabu ya Middlesbrough baada ya kutokea nchini China katika klabu ya Tianjin Teda.