Sambaza....

Nahodha wa timu ya kandanda ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ Mikel John Obi kwa mara nyingine ameachwa katika kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na michezo miwili ya Kimataifa.

Obi ambaye alikiongoza vyema kikosi cha Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni nchini Russia ameachwa na sababu za kuachwa kwake hazijawekwa wazi.

Obi hajaichezea Nigeria toka kwenye fainali za Kombe la Dunia na aliachwa kwenye kikosi kilichocheza mechi mbili dhidi ya Libya na sababu zilitajwa kuwa ni kumpa nafasi ya kuuguza majeraha aliyokuwa ameyapata.

Lakini toka kipindi hicho amekuwa akicheza mara kwa mara katika timu yake ya Tianjin Teda ya China hivyo kuachwa katika kikosi cha sasa cha kocha Gernot Rohr kumeibua maswali mengi kuliko majibu.

Kikosi kilichoitwa.

Makipa: Francis Uzoho (Elche/ESP), Ikechukwu Ezenwa (Enyimba), Daniel Akpeyi (Chippa United/RSA).

Walinzi: Olaoluwa Aina (Torino/ITA), Adeleye Aniyikaye (IfeanyiUbah), Semi Ajayi (Rotherham United/ENG), Bryan Idowu (Lokomotiv Moscow/RUS), William Ekong (Udinese FC/ITA,), Leon Balogun (Brighton & Hove Albion/ENG,), Kenneth Omeruo (CD Leganes/SPA), Jamilu Collins (SC Padeborn 07/GER).

Viungo: Oghenekaro Etebo (Stoke City FC/ENG), John Ogu (Hapoel Be’er Sheva/ISRl), Mikel Agu (Vitoria Setubal FC/POR).

Washambuliaji: Ahmed Musa (Al Nassr/KSA), Kelechi Iheanacho (Leicester City/ENG), Moses Simon (Levante/ESP), Victor Osimhen (Royal Charleroi/BEL), Odion Ighalo (Changchun Yatai/CHN), Alex Iwobi (Arsenal/ENG), Samuel Kalu (Bordeaux/FRA), Isaac Success (Watford/ENG); Samuel Chukwueze (Villarreal/ESP).

Mbadala : Henry Onyekuru (Galatasaray/TUR), Chidozie Awaziem (Porto/POR), Nyima Nwagua (Kano Pillars), Sunday Adetunji (Enyimba), Junior Lokosa (Kano Pillars).

Nigeria watacheza na Afrika Kusini November 17 katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 kabla ya baadae kucheza na Uganda November 20 mjini Asaba katika mchezo wa Kirafiki.

Sambaza....