Sambaza....

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Orlando Pirates, Bernard Morrison amefichua sababu muhimu zinazomfanya kocha wa Young Africans, Nasreddine Nabi kufaa kuinoa Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.

Kocha Nasreddine Nabi amekuwa akihusishwa na kazi ya ukocha mkuu wa Kaizer Chiefs, ambayo kwa sasa inashikiliwa na Arthur Zwane. Raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi amekuwa kwenye usukani wa Young Africans tangu Aprili 2021.

Mpaka sasa Nabi ameiongoza Yanga kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, mawili ya kombe la FA na mawili ya Ngao ya Jamii. Pia ameiwezesha Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.

Nasraddine Nabi akiwa na benchi zima la ufundi la Yanga.

Bernard Morrison ambaye alicheza katika Ligi ya PSL kwa muda anaamini uzoefu wa Yanga unakoleza uvumi wa kocha Nasreddine Nabi kwa kazi yoyote yenye presha. “Anajua kwamba kwa klabu hizi kubwa, sare moja tu, kupoteza moja umekwenda. Kwa hivyo anajua shinikizo linalokuja nayo,” Morrison aliambia FARPost.

“Sasa amekuwa hapa kwa karibu miaka miwili. Nafikiri anaweza kwenda kwenye vilabu au klabu nyingine yoyote kubwa nchini Afrika Kusini. Anajua shinikizo analopaswa kutoa, kama sivyo watachukua nafasi yake. Kwa hiyo lazima awe tayari kwa lolote litakalomjia.”

Kaizer Chiefs itatumai kumshawishi Nasreddine Nabi kujiunga nao kabla ya msimu wa 2023/24. Msimu uliopita bila shaka ulikuwa wa mbaya kwao huku wakishindwa kuwakabili wapinzani wao Mamelody Sundows. Licha ya uwekezaji mkubwa kwa Zwane, klabu ilimaliza Ligi bila kombe lolote.

Nasraddine Nabi akiwa na kombe la FA baada ya kuifunga Azam Fc katika fainali.

Amakhosi walimaliza msimu wakiwa katika nafasi ya tano kwenye DStv Premiership huku wakishuhudia Mamelody wakiendeleza utawala wao katika Ligi ya PSL. Chiefs pia wamekosa nafasi ya kuiwakilisha nchi Kimataifa msimu ujao.

Mkataba wa Nabi na Yanga umemalizika huku viongozi wa Yanga wakikiri mkataba huo umemalizika na wapo katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba Mtunisia huyo.

Baada ya kumalizila kwa mchezo wa fainali akiiezea hatma yake Nabi alisema “Lakini kuhusu mimi naomba hili litajulikana hapo baadaye kwasasa tunasherehekea ubingwa tulioupata, Wanayanga tunapaswa kusherekea haya na mengine yatafuata baadaye, kwani hakuna kitu kinachoweza kujificha.”

Sambaza....