Sambaza....

Kiungo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Abdalla Hamis amejiunga na timu ya Orapa United FC ya nchini Botswana kwa mkataba wa miaka miwili, imethibitishwa.

Hamisi ambaye aliichezea Tanzania Bara ‘Kilimanjaro stars’ kwenye michuano ya ukanda wa Afrika Mashaiki na Kati ‘’CECAFA’ iliyofanyika nchini Kenya mwaka 2017 amejiunga na Orapa FC akitokea Bandari FC ya Kenya.

Taarifa zinasema kuwa sababu kubwa ya Hamisi ambaye ni mzaliwa wa mkoani Mara kuelekea Botswana na kutopata nafasi ya kucheza kwenye timu yake ya Bandari tofauti na ilivyokuwa wakati akiitumikia Sony Sugar FC ambayo ndiyo ilimfanya kuitwa Taifa Stars.

“Nina furaha kwa sababu nimejiunga na mojawapo ya timu kubwa sana nchini Botswana, mambo hayakwenda sawia kama nilivyodhani nilipokuwa na Bandari, na ningependa kuwashukuru kwa muda wote ambao nilikuwa pale, ninaelekea kwenye mazingira tofauti kidogo hivyo ninahitaji kwanza kuyazoea lakini naamini nitakuwa na wakati mzuri nitakapokuwa pale,” Hamisi ameuambia mtandano wa Futaa wa nchini Kenya.

Hamisi ambaye mbali ya kuichezea Sony Sugar na Bandari lakini pia amewahi kuichezea Muhoroni Youth zote za nchini Kenya na sasa anaelekea nchini Botswana.

Mara ya mwisho alikuwa na timu ya Bandari kwenye michuano ya SportPesa iliyofanyika hapa nchini na kuisaidia timu hiyo kucheza hatua ya fainali lakini walipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Kariobangi Sharks.

Anakwenda kujiunga na Orapa ambayo imemaliza nafasi ya tatu msimu uliomalizika kwenye ligi inayoshirikisha jumla ya timu 16.

Sambaza....