Sambaza....

Akiwa kwenye kikosi cha USM Alger Tumisang Orebonye Mchezaji wa kimataifa wa Botswana  anajivunia mafanikio ya USM Alger ya kombe la Shirikisho la CAF na amefichua kinachoifanya mafanikio hayo kuwa ya kipekee zaidi.

USM Alger iliweka historia baada ya kushinda taji lao la kwanza kabisa la Afrika. Waliishinda Young Africans ya Tanzania kwa kanuni ya bao la ugenini katika fainali ya kombe la shirikisho la CAF 2022/23 kwa mikondo miwili.

Ingawa walikumbana na kichapo cha 1-0 nyumbani, matokeo ya jumla ya 2-2, yaliyotokana na ushindi wao wa 2-1 wa mkondo wa kwanza yaliwawezesha kutwaa taji hilo. 

USM Algier mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu 2022/2023.

Akiwa ameweka historia, Tumisang Orebonye pia amekuwa mchezaji wa kwanza wa Botswana kushinda taji la CAF la kombe la shirikisho. Lakini kilichofanya mafanikio hayo kuwa matamu zaidi ni ujumbe wa kufurahisha aliopokea kutoka kwa Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune. “Leo nilifanikiwa kupeana mkono na rais wa Algeria na akaniambia kuwa mimi ni mmoja wa wachezaji bora katika timu,” alisema Orebonye akiiambia FarPost.

“Rais aliniambia kuwa mimi ni mpiganaji. Alikuwa akitazama mchezo wetu wa mwisho.” Tumisang Orebonye alichangia bao moja na asisti mbili katika mechi 12 za kombe la Shirikisho la CAF alizocheza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye anacheza kama mshambuliaji wa kati wa USM Alger yuko kwenye kilele cha mafanikio kufuatia mafanikio hayo.

Tumisang Orebonye.

“Nina furaha sana kwamba mimi ni Mtswana wa kwanza kushinda taji hili la CAF na pia kuwa sehemu ya timu iliyoweka historia nchini Algeria. “Kuwa timu ya kwanza kushinda taji hapa. Sina maneno ya kuelezea kile ninachohisi sasa lakini ninaishi wakati huu na nina furaha kwamba nilifanikisha hili, “aliiambia FARPost.

Orebonye alijiunga na USM Algier katika usajili wa dirisha dogo akitokea timu ya Morocco Olympique Khouribga ambao nao walimsajili akitokea kwao Botswana kwa wababe Township Rollers. 

Sambaza....