Sambaza....

Mlinda mlango namba moja wa klabu ya Simba Aishi Manula ameondoka nchini na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya nyama za paja aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Ihefu.

Manula alipata majeraha katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ihefu FC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Aprili 7 na kumfanya kukaa nje kwa muda mrefu na kukosa michezo ya msimu mzima iliyobaki.

Kwa majeruhi hayo yalimfanya kukosa michezo muhimu ya Simba msimu huu kama ile ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, nusu fainali dhidi ya Azam Fc ta kombe la FA na mchezo dhidi ya Yanga katika Ligi.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo ambaye ameongozana na Manula amesema mlinda mlango huyo atafanyiwa upasuaji ikiwa ni sehemu ya matibabu yake. Kagabo amesema watafikia katika Jiji la Johannesburg na ndipo upasuaji na matibabu yake yatafanyika.

“Tunaondoka kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya mlinda mlango wetu Aishi. Matibabu yake yatahusisha upasuaji kwahiyo kuhusu atakuwa nje kwa muda gani itategemea na upasuaji huo,” amesema Dk. Kagabo.

Kwa kilindi chote hicho ambacho Simba ilikua inamkosa Manula langoni alikua anakaa kipa namba tatu Ally Salim na si Benno Kakolanya mlinda mlango namba mbili aliyetarajiwa kukaa langoni.

Sambaza....