Sambaza....

Kocha wa timu ya soka ya Mbeya City ya jijini Mbeya ‘wanakomakumwanya’ Ramadhan Nswanzurimo amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa wasijisikie vibaya kutoka vichapo vitatu mfululizo vya ligi kuu soka Tanzania Bara.

Nswanzurimo amesema mpaka sasa Mbeya City ndio timu pekee ambayo imecheza na Bingwa na kaimu Bingwa wa ligi kuu msimu uliopita pamoja na Bingwa wa kombe la Shirikisho hivyo matokeo hayo ni kama changamoto kwao kuelekea michezo mingine.

“Mashabiki wasivunje moyo, timu ipo vizuri, timu inaonesha picha nzuri, kumbuka kwamba tumecheza na mabingwa, tumecheza na namba mbili na bingwa wa FA Cup, tunategemea kwamba kwetu ilikuwa test kubwa na imetupa picha nzuri na tutafikia wakati tutakuwa katika kiwango kizuri,”

“Kwenye game ya kwanza tulicheza na timu ambayo mbali na kuwa makamu bingwa lakini pia iliweka kambi nchini Uganda, tukaja kucheza mechi ya pili na timu ambayo imeweka kambi nchini Uturuki hivyo matokeo haya wote tuyachukulie kama sehemu ya kujifunza,” ameongeza.

Mbeya City katika mchezo wao wa kwanza walichezea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, kabla ya kupoteza mbele ya Mnyama Simba kwa mabao 2-0 kabla ya mchezo wa tatu kuachia pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kukubali kichapo cha mabao

Sambaza....