Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wameingia makubaliano na benki ya NMB ya kutoa kadi maalum kwa mashabiki wa Simba ambazo zitakua zinatoa pia huduma za kibenki.

Katika hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ikishihudiwa na mashabiki kibao wa Simba waliojitokeza katika uzinduzi huo. Kwa upande wa Simba katika hafla hiyo iliwakilishwa na Mtendaji mkuu Imani Kajula, Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtazar Mangungu pamoja na wajumbe wa bodi.

Akizungumzia ushirikiano huyo Imani Kajula alisema “Simba ni klabu namba saba kwa ubora Afrika na NMB ndio benki bora nchini na huu utakua muunganiko bora zaidi na ndio maana tunafanya mambo hadharani kabisa hatujifichi,” alisema na kuongeza.

“Mashabiki wa Simba wanahitaji kupata faida ya ushabiki wao na hivyo sisi Simba ndio klabu ya kwanza kabisa Tanzania na Afrika kuwa na akaunti yake ya benki yaani Simba akaunti.”

Imani Kajula, Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba.

Kutakua na kadi za mashabiki ambazo zitajumuisha akaunti za Platinum, akaunti za watoto na Simba queen akaunti. Na zote hizo zitakua na bima ambazo zitafunguliwa kwa elfu tano pekee.”

Kaimu afisa mtendaji mkuu wa NMB Filbert Mponzi akizingumzia ushirikiano huo alisema “Niwapongeze kwa kuwa klabu namba 7 kwa ubora Afrika na ndio maana leo tumeamua kushirikiana na nanyinyi, benki bora imekutana na klabu bora.”

“NMB ipo nchi nzima na Simba ina mashabiki Tanzania nzima hivyo tutafika mbali katika ushirikiano huu. Shabiki wa Simba utapata kadi ya NMB Master card ambazo zitakua na rangi maalum za Simba.

Ni kadi ambazo zitakutambulisha kama shabiki wa Simba lakini pia zitatumika katika matumizi ya kawaida ya kibenki.”

Sambaza....