Kulikuwa na tetesi kuwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga , Mwinyi Zahera anatakiwa tena na viongozi wa Yanga arudi kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa Kihistoria.
Akizungumza na kituo cha habari cha Global Online TV kuhusu uwezekano wa yeye kurudi Yanga siku moja amedai kuwa inawezekana kurudi Yanga Lakini mpaka vitu vibadilike .
“Mimi siwezi kurudi Yanga kama timu itaendelea kuendeshwa hivi kiuanachama ambao hawana maono , nitarudi Yanga mpaka kuwe na viongozi wenye maono .
“Kukiwa na viongozi wanaoona mbali nitarudi , Lakini kwa sasa hapana siwezi kurudi Yanga kwa sababu hakuna viongozi wenye maono “- alisema Mwinyi Zahera .
Mwinyi Zahera alidai kuwa kwa jinsi walivyo GSM wanaonekana wana maono na wanaona mbali . Hivo kama wakichukua timu anaweza kurudi kwenye klabu hiyo.
“GSM wana maono ya mpira , wanaona mbali kama wakichukua timu ninaweza kurudi Yanga kufanya kazi , hivi hivi siwezi kurudi Yanga , nitarudi Yanga kama kukiwa na mabadiliko”- alimalizia kocha huyo wa zamani wa Yanga.