Simbasc ndio kinara wa ligi ikiwa na point 58 wakifwatiwa na Yanga yenye point 47 huku ikizidiwa michezo miwili na Simba.
Baada ya kuukosa ubingwa kwa takribani miaka 5 klabu ya Simba ina nafasi nzuri ya kua bingwa katika msimu huu kutokana na form nzuri walionayo.
Benchi la ufundi la Simbasc limekua likitumia mfumo wa 3:5:2 baada ya kuja kwa benchi jipya la ufundi likiongozwa na Pierre Lenchentre akisaidiwa na Masoud Djuma.
Kueleka mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga ningeipanga hivi timu yangu:
Katika mfumo wa 3:5:2
1. Aishi Manual, 2. Shomari Kapombe, 3. Asante Kwasi, 4. Juuko Mursheed, 5. Yusuph Mlipili, 6. Erasto Nyoni, 7. Said Ndemla, 8. Jonas Mkude, 9. John Bocco, 10. Emmanuel Okwi 11. Shiza Kichuya.
Sub: Said Nduda, Mohamed Hussein, Salim Mbonde, James Korea, Mdhamiru Yasin, Nicholas Gyan, Laudit Mavugo!
Mfumo ungefanyaje kazi:
Walinzi wa kati:
Katika mfumo wa 3 : 5 : 2 kwenye sehemu ya ulinzi itakua na Yusuph Mlipili Erasto Nyoni na Juuko Mursheed wakiwa na jukumu la kucheza kama mabeki wa kati wa mwisho.
Wing-back:
Hapa kuna Shomari Kapombe upande wa kulia na Asante Kwasi upande wa kushoto. Kazi kubwa ya hawa wawili ni kusaidia mashambulizi na pia ukabaji pindi timu inaposhambuliwa.
Kasi, uwezo wa kumiliki mpira ukabaji na upigaji wa pasi za mwisho kwa ufasaha mkubwa ndio silaha kubwa ya mfumo huu katika maeneo ya pembeni ya uwanja.
Viungo:
Kiungo wa ukabaji ni Jonas Mkude na viungo washambuliaji ni Said Ndemla na Shiza Kichuya . Ambao hawa ndio watakaokua na amri ya mchezo (game control).
Kwa uzoefu walio nao wa mechi kubwa zenye presha hakuna Shaka ndio chaguo sahihi katika mchezo. Kasi na uwezo wa kupiga pasi za mwisho kwa Said Ndemla na Shiza Kichuya zitaisadia SimbaSc kupenya katika ngome za Yanga.
Washambuliaji:
Hakika ni eneo rahisi katika upangaji wa timu katika kikosi cha Simba. John Bocco na Emmanuel Okwi ndio chaguo sahihi kwa wakati sahihi wa mchezo wa kesho.
Uwezo wa kucheza mipira ya juu, kasi na uzoefu walionao hakika hawa ndio watakaoipa SimbaSc ushindi. Mpaka sasa wana magoli zaidi ya 30 ni jinsi gani walivyo kwenye nafasi nzuri ya kupachika mabao kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
Mabadiliko Ikiwa Timu Haijapata Matokeo Mpaka Kipindi Cha Pili:
Wakati mwingine kwenye mpira mambo huenda tofauti kama unavyopanga. Mpaka kipindi cha pili ikiwa timu ipo tayari mababidiliko ya haraka ni kumtoa Yusuph Mlipili na kumuingiza laudit Mavugo na kurudi katika mfumo wa 4:4:2 na pia kumuingiza Mdhamiru Yasini kuchukua nafasi ya Said Ndemla.
Lakini pia kujilipua zaidi ningemtoa Shomari Kapombe na kumuingiza Nicholas Gyan ili kuongeza kasi pembeni.
Mabadiliko Ikiwa Timu imepata matokeo katika kipindi cha pili:
Baada ya timu kupata ushindi walau wa goli moja au mawili njia sahihi iliyobaki ni kulinda ushindi uliopo.
Ntamtoa Said Ndemla katika kiungo na kumuingiza Mdhamiru Yasini huku pia nikimpumzisha Shiza Kichuya/John Bocco na kumuingiza uwanjani James Kotei!