NI miezi tisa hadi kumi imesalia kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kiungo-mshambulizi Ibrahim Ajb klabuni Yanga SC. Ndani ya miezi 15 ya mwanzo , Ajib bado hajafanya mambo makubwa kama ilivyotarajwa wakati anasajiliwa kutoka Simba SC katikati ya mwaka uliopita, lakini kwa umri wake inaonyesha bado ana weza kufika kiwango cha juu zaidi kiuchezaji ambacho bado hakijaonekana.
Kama ningekuwa meneja wa kinara huyo wa ‘usaidizi magoli’ katika ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, ningemshauri kubaki Yanga na kusaini miaka miwili zaidi. Kwa mchezaji U25 wakati mwingine ili kufkia kiwango cha juu zaidi kiuchezaji anapaswa kutulia mahali na kucheza mpira.
Ajib alicheza Simba kwa misimu minne, lakini wakati huo alikuwa bado si mchezaji aliyekomaa kimpira. Kwa sasa anahitaji mahala ambako atacheza mara kwa mara ili kuendelea kukua kiuzoefu, na hata kama ni kweli soka ni kazi yake lakini anapaswa wakati mwingine kufikiria kusonga mbele zaidi na si kila baada ya misimu miwili kusubiri pesa za Yanga au Simba.
Alishacheza Simba ( miaka minne) n na kama atacheza na Yanga kwa miaka minne mingine itakuwa ni vizuri lakini kwa kuwa bado ana nafasi kiumri, kubaki Yanga kwa miaka miwili ijayo si tu kumsaidie kupata pesa bali anatakiwa kutazama nafasi yake ya kukua kimpira. Ni msimu wa sita huu kwake akicheza ligi kuu Tanzania bara hivyo tayari kwa mchezaji mwenye matamanio zaidi anajiona amechelewa.
Ili kuondoa presha ya kutokuja kufanya maamuzi sahihi wakati mkataba wake utakapomalizika Juni 2019, ni vyema uongozi wa Yanga ukamuuliza kocha wao Mcongo, Zahera Mwiny kama anamuhitaji zaidi Ajib na ikiwa hivyo wafungue sasa mazungumzo ya kumsaini tena kwa miasimu miwili ijayo ama mitatu.
Kwa mtazamo wangu, Ajib anaihitaji zaidi Yanga ili kuendelea kukua kimpira, lakini na Yanga nao naona kabisa wakimuhitaji mchezaji huyo namba kumi. Kubaki Yanga kwa misimu walau miwili zaidi kwa Ajib kutaisaidia mno klabu na mchezaji na katika hili Yanga nao hawatatakiwa ‘kuwa wachoyo.’ Ajib ni mume hivyo ni mtu anayejenga familia yake kwa sasa, lazima alipwe vizuri kutokana na kazi yake.
Yanga ‘wafungue pochi’ sasa kwa sababu watatoa bila presha ifikapo Juni mwakani na Ajib naye anapaswa kujitazama na kujipa thamani anayoona inastahi lakini hadi sasa hajafikia thamani ile ya aliyoingilia Yanga Juni, 2017 akitokea kwa mahasimu wao Simba. Huu ndiyo wakati sahihi wa Ajib na Yanga kuanza kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na kila upande utanufaika.