Emmanuel okwi na John Bocco wapo moto kwelikweli katika ufungaji kwenye ligi kuu bara (VPL ). Wawili hao wamefanikiwa kuipa ushindi timu yao Simbasc dhidi ya Tanzania Prisons wa mabao mawili kwa bila, huku Bocco na Okwi wakifunga kila mmoja na kuwafanya kufikisha mabao 33 wenyewe, Okwi (19) Bocco (14).
Vodacom Premier league (VPL) msimu wa 2016/2017 inazihusisha timu 16 kutoka mikoa mbalimbali huku Simbasc akiwa ndio kinara. Katika timu zote hizo ni timu mbili pekee ambazo hazijakutana na makali ya ufungaji wa kinara wa mabao Emmanuel Okwi na msaidizi wake John Bocco.
Timu tatu za Lipuli fc ya Iringa, Stand utd ya Shinyanga na Yangasc ya Dar es salaam ndioo pekee hazijafungwa na Wawili hao wanaoongoza katika chati ya ufungaji bora.
Mchezo kati ya Simba dhidi ya Lipuli uliisha kwa kufungana bao moja kwa moja wakati bao la Simba likifungwa na mkongwe Mwinyi Kazimoto. Lakini Lipuli wanakwenda kukutana na Simbasc katika raundi ya pili weekend hii. Pia timu ya Yangasc imenusurika na combination hii kwani Mchezo wa kwanza uliisha kwa sare ya bao moja kwa moja huku goli la Simbasc likifungwa na Shiza Kichuya. Huku stand wakifungwa mabao mawili na Kichuya&Mavugo huku wakipata sare ya mabao matatu kwa matatu huku mabao ya Simba yakifungwa na Gyan, Mavugo& Kwasi.
Timu zilizofungwa na Combination ya Bocco & Okwi:
- Prisons mabao 3
- Mbeya city mabao 2
- Mtibwa sugar mabao 2
- Njombe Mji mabao 3
- Mbao fc mabao 2
- Mwadui mabao 5
- Azamfc goli 1
- Ruvu Shooting mabao 6
- Majimaji mabao 4
- Kagera sugar goli 1
- Singida utd mabao 2
- Ndanda fc mabao 2