Kumekuwa na mgogoro kati ya uongozi wa Yanga pamoja na kiungo wao ambaye ni nahodha wa timu hiyo Papy Kabamba Tshishimbi. Mgogoro huu unatokana na pande zote mbili kuvutana kuhusiana na suala la kuongeza mkataba mpya.
Mkataba kati ya Papy Kabamba Tshishimbi na Yanga unamalizika tarehe 12/08/2020 . Uongozi wa Yanga umempa Papy Kabamba Tshishimbi siku kumi na nne ili kuongeza mkataba tofauti na hapo wataachana naye.
Kama Papy Kabamba Tshishimbi ataachwa na Yanga kuna tetesi za Simba kumtaka Papy Kabamba Tshishimbi kwenye kikosi chao. Kuna vitu vitatu ambavyo vinaonesha Simba kutonufaika na Papy Kabamba Tshishimbi kama wakiamua kumsajili.
1: JERAHA LA GOTI
Msimu uliomalizika wiki iliyopita Papy Kabamba Tshishimbi hakupata muda mrefu wa kuitumikia timu yake ya Yanga kutokana na majeraha ya goti ambayo alikuwa anakabiliwa nayo kwa kiasi kikubwa.
Alitibiwa na akarudi uwanjani lakini hakufanikiwa kurudi kwenye kiwango chake kikubwa ambacho tulizoea kumuona. Inaonesha jeraha lake la goti limerudisha nyuma kasi yake uwanjani.
Kwa hiyo kama Simba watafanikiwa kumsajili Papy Kabamba Tshishimbi hawatonufaika na kasi yake ya zamani kwa sababu kwa sasa kasi yake imepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na zamani.
2: UMRI WAKE
Frank Domayo alipata jeraha la goti wakati akiwa anachezea Yanga , Yanga wakashindwa kumtibu lakini Azam FC walimsajili akiwa na majeraha yake na kumtibu. Frank Domayo alipona kwa sababu ya umri wake wa wakati huo kuwa mdogo .
Hii ni tofauti na Papy Kabamba Tshishimbi ambaye umri wake kwa sasa ni mkubwa , umri ambao haukupi nafasi ya kumrudisha kwenye kiwango chake kikubwa kama baada ya kutibiwa goti lake.
3: UWEPO WA FRAGA NA MKUDE
Kwenye nafasi ambayo Papy Kabamba Tshishimbi anacheza kuna wachezaji wawili wa kiwango cha juu ndani ya Simba ambao ni Jonas Mkude na Mbrazil Fraga. Kwa hiyo ni hasara kubwa kumleta mchezaji ambaye umri wake umeenda na ana majeraha ya goti huku ndani ya kikosi kuna wachezaji wawili wenye kiwango cha juu.