Sambaza....

Baada ya miaka 14 Mtibwa Sugar inatarajiwa kurejea katika michuano ya Kimataifa na mara hii itakuwa ikiumana na Northern Dyamos ya Ushelisheli katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya awali.

Mchezo huo wa Kimataifa Utafanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam ambapo tayari viingilio vimetajwa huku kiingilio cha bei ya chini kabisa ikiwa ni shilingi Elfu mbili.

Afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligalambwike amewaomba Watanzania bila kufuata ushabiki wao kujitokeza kwa wingi katika mchezo na kuwashangilia muda wote ili wao Kama wawakilisha wa nchi waweze kufanya vizuri na kusonga mbele.

“Tunawakaribisha Watanzania wote bila kujali unaipenda klabu gani hapa nchini, kuja kwenye uwanja wa Azam Complex kuishangilia Mtibwa, sisi ndo wawakilishi hivyo ni vyema tukiwaona watanzania kwa umoja wao wakija kutushangilia,” amesema.

Ikumbukwe Mtibwa inashiriki michuano hiyo baada ya kumaliza adhabu ya shirikisho la soka Afrika ‘CAF’ baada ya kufungiwa misimu mitatu kutokana na kushindwa kusafiri mwaka 2004 kwenda Afrika Kusini kucheza na Santos baada ya kichapo cha mabao 3-0 nyumbani, huku wakisingizia ukata ndio sababu ya kushindwa kusafiri.

Mtibwa Sugar watahitaji kushinda kwa mabao Mengi zaidi Ili kujiwekea nafasi nzuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika baadae nchini Ushelisheli.

Sambaza....