Sambaza....

Rasmi Leo tarehe 8/10/2018 klabu ya Simba imesitisha mkataba na aliyekuwa kocha msaidiizi wa klabu hiyo Masoud Djuma Irambona.

Akizungumzua katika makao makuu ya klabu ya Simba, kaimu Raisi wa Simba amedhibitisha kwa kusema kuwa;

“Kwa niamba ya klabu sisi tunamshukuru sana kwa huduma zake, tumekaa naye vizuri na tumefanya naye kazi kwa karibu”.

” Kwa sisi ambao tumefanya naye kazi kwa kariɓu tunafahamu uwezo wake ni mwalimu mzuri, lakni kama unavyofahamu kila jambo lina mwisho wake, sisi kwa faida ya klabu yetu, tumefanya makubaliano kwa faida ya panɗe zote mbili tumevunja mkataba huu ili tuweze kuendelea. ,

” Sisi tumemfungulia mlango Masoud kwa roho safi na tuseme kwamba huenda hii ndiyo ikawa bahati yake huko mbele ya safari kwa sabaɓu sisi tunamini ni mwalimu mzuri na tunaami atatapa klabu kubwa zaidi ya Simba na Mungu akipenda Masoud anaweza kurudi Tnzania kufundisha klabu ya Simba.

” Wanachama na wapenzi wa klabu yetu tunawaomba watulie”. Pia Mwalimu Masoud Djuma Irambona alipata nafasi ya kuzungumza yafuatayo;

“Walinipa nafasi ya kufika Simba , sikuwa najua kama nitafika Smba lakini leo hii Mungu amenijalia nimefika Simba.

“Watu wengine wa kuwashukuru nafikiri ni wanachama wa simba bila kuwasahau zaidi mashaɓiki wangu nawapenda sana .

” Kila jambo lina mwanzo na mwisho. Timefika makubaliano ya klabu na mimi juu ya maslahi mazuri ya Simba kwenye ligi na kwenye mashindano mengine. Nafikiria kila lenye mwanzo lina mwisho”.

Naye msemaji wa klabu ya Simba alipata nafasi ya kudhibitisha habari hii kwa niamba ya klabu.

“Ndugu wanachama ,washabiki na wapenzi wa Simba kwa niaba ya uongozi wa Simba Sc ningepenɗa kwa masikitiko nitangaze rasmi kwamba. Klabu ya simba na kocha wetu msaiɗizi Masoud Djuma Irambona tumesitisha mktaba wetu kiungwana kwa yeye kuendelea kuwa kocha wa Simba.

” Tumefanya hivi kwa kuangalia maslahi ya pande zote mbili, upande wa klabu ya Simba na Upande wa Kocha Masoud.

Kimsingi Masoud ameafikiana na sisi tumefiafikiana kiungwana sisi kama simba tunamtakiwa kila la kheri”.

Sambaza....