Sambaza....

Ligi imesimama baada ya janga la Dunia la ugonjwa wa corona na hivyo kupelekea kila mtu kubaki nyumbani kwake ili kuchukua tahadhari ya kuzui kuenea zaidi ugonjwa huo.

Lakini ligi ikiwa imesimama tayari harakati za usajili zimeanza kimyakimya huku vigogo wa nchi Simba na Yanga wakianza kutunisihiana misuli na kuanza kuviziana kwa kila mmoja akitaka kubomoa ngome ya mwenzake na kuujimarisha kikosi chake.

Vuguvugu hilo likiwa limepamba moto tayari kuna baadhi ya wachezaji wameanza kuhusishwa na kuvihama vilabu vyao na kutimkia kwa wapinzani wao.

Said Hamis Ndemla.

Said Hamis Ndemla ambae mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu amekua akiwindwa kwa muda mrefu na Yanga huenda sasa ukawa wakati sahihi wa kutimkia Jangwani na kuendelea kuonyesha makali yake akiwa na jezi namba 13 za njano na kijani.

Tangu msimu uliopita Ndemla alikua aingie katika kikosi cha Yanga lakini inasemekana mwalim Mwinyi Zahera ndie alieweka kizuizi kwa kiungo huyo mkali wa mashuti na hivyo kuwafanya viongozi wa Jangwani chini ya Mwenyekiti Msolla kufyata mkia na kuachana nae.

Upande wa pili kuna Papy Tshishimbi ambae amekiri mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni hivyo yupo huru kuzungumza na timu yoyote ili kuweza kujiunga nao katika msimu ujao.

Papy Kabamba Tshishimbi.

Simba wameonyesha matamanio na kiungo huyo Mkongo huku msemaji wao Hajji Manara akikiri hadharani kuhusudu uwezo wake akisema ni moja ya “box to box midfielder” bora kuwahi kuwashuhudia katika VPL.

Muda utaongea na hitimishi la yote haya tutaona katika dirisha la usajili ni nani atakua mwamba zaidi ya mwenzake, ni Simba au Yanga atakaeibuka kinara na kuweza kuinasa saini ya Ndemla au Tshishimbi.

Sambaza....