Kocha wa Azam Fc, Etiene Ndayiragije ametoa sababu za kupoteza mchezo mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba SC katika uwanja wa taifa.
Ndayiragije amesema kuwa, mechi ya marudiano dhidi ya Fasil Kenema katika michuano ya Shirikisho Afrika ndio sababu kubwa kwa Azam kukubali kichapo cha goli 4-2 kutoka kwa Simba.
‘… hata matokeo tuliyoyapata kwa Simba ni kutokana na kuweka nguvu nyingi katika mchezo wa marudiano, kwa kuwa michuano hiyo ipo katika malengo ya klabu…”
Licha ya kupoteza mchezo huo, Ndayiragije amekiri kuwa mchezo dhidi ya Simba ulikuwa na maana kubwa kwake na kikosi chake, kwani umewapa somo na kumempa fursa ya kurekebisha baadhi makosa na kukazia zaidi baadhi ya vitu.
Katika mchezo huo, Azam ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Shabani Iddi Chilunda kabla ya Abdul Shiboub kuingia kambani mara mbili, Clatus Chama mara moja na Fransis Kahata kuhitimisha idadi ya magoli. Goli la pili la Azam lilifungwa na Nahodha katika mchezo huo, Frank Domayo Chumvi.
Aidha katika hatua nyingine, Kocha Ndayiragije amewataka mashabiki wa Azam na wadau wa Soka nchini kujitokeza kwa wingi Siku ya Jumamosi kuishangilia Azam katika mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Fasil Kenema kutoka Ethiopia.
‘…tuko nyumbani tunaimani kuwa ujio wa mashabiki utatuongezea nguvu, najua kuwa ushindi upo upande wetu lakini tunahitaji dua za mashabiki na hamasa kutoka kwao…’
‘…tumejiandaa vya kutosha dhidi ya Kenema, na tulikuwa tukiangalia afya za wachezaji waliokuwa wamepata majeraha kidogo na naona kama wengi wako vizuri na tunamshukuru Mungu kwani tutakuwa na kikosi kamili..’
Ikumbuykwe kuwa katika mchezo wa awali uliopigwa
kule nchini Ethiopia, Azam Fc walikubali kipigo cha goli 1-0 hivyo wanahitaji
kufanya vizuri zaidi katika mchezo wao wa marudio utakaochezwa pale Chamazi
Complex siku ya jumamosi.