Licha ya kuwasiliana na Nasraddine Nabi kwa muda mrefu lakini klabu ya Kaizer Chiefs haikumpa kazi Nasraddine Nabi na hatimae Ntseki akipata nafasi hiyo.
Mapema wiki hii, taarifa liliripoti kwamba Nabi aliwakataa Kaizer Chiefs kwa sababu hawakuwa tayari kukubaliana na ombi lake la kuwa na wakufunzi wake binafsi.
Sasa kwa mujibu wa KickOff.com kocha huyo wa Tunisia huenda akapata kibarua kizuri zaidi huku wababe wa Morocco Wydad Casablanca wakinyemelea.
“Sasa imebainika kuwa kocha huyo mwenye miaka 57 ameelekeza umakini wake katika soko la Afrika Kaskazini akiwa tayari ameshawasiliana na Wydad Casablanca ya Morocco. Wydad wameachana na Sven Vandenbroeck baada ya kushindwa kushinda ligi ya ndani na Mabingwa hao wa CAF kumemaanisha Mbelgiji huyo anaonekana kutolewa macho,” kilisema chanzo hicho.
Wydad Casablanca ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Sven Vandebroeke ilipoteza katika fainali ya Ligi ya mabingwa Africa baada ya kufungwa na Al Ahly ya Misri.
Kwasasa tayari Sven ambae aliifundisha Simba December 2019 mpaka January 2021 anatarajiwa kutambulishwa katika klabu ya CD Belouzdaid ya nchini Algeria kama kocha wao mpya.