Hapana shaka kwa sasa Simba ina safu imara ya ushambuliaji kwa sasa kwa sababu ina washambuliaji watatu ambao ni bora kwa sasa, je yupi kati ya hawa ni bora zaidi kuzidi mwenzake ? Tuangalie maeneo yafautayo ambayo yatatupa sura halisi ya yupi ni bora zaidi ya mwenzake.
MIPIRA YA JUU
Ukitazama kati ya hawa watatu, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco. Kuna wachezaji wawili pekee ambao wanauwezo wa kucheza vizuri mipira ya juu, nao ni Meddie Kagere na John Bocco.
Mfano ukitazama kwenye mechi dhidi ya Mwadui , magoli mawili kati ya magoli matatu ya Simba yalifungwa kwa kichwa, na wafungaji walikuwa wawili (John Bocco na Meddie Kagere). Emmanuel Okwi anazidiwa kwa kiasi kikubwa sana na hawa wawili kwenye mipira ya juu.
KUUNGANISHA MASHABULIZI
Ukitazama vizuri kati ya hawa watatu, John Bocco huwa ni mzuri katika kuunganisha mashambulizi ambayo huzalisha magoli, mfano katika mechi dhidi ya mwadui goli la Mzamiru Yasin alikuwa kiunganishi mzuri wa goli lile , hivo hivo hata kwenye mechi dhidi ya Al Ahly goli la Meddie Kagere yeye ndiye aliyeunganisha shambulizi lililozaa goli.
KUTENGENEZA UWAZI
Wote watatu huwa wanawalazimisha mabeki kutengeneza uwazi eneo la nyuma. Ila huwa wanatofautiana jinsi ya kuwalazimisha mabeki wa timu pinzani kutengeneza uwazi eneo la nyuma.
Mfano, John Bocco yeye husimama katikati ya mabeki wawili muda mwingi. Unaposimama katikati ya mabeki wawili, mabeki huwekeza muda mwingi kwako, hivo kuacha uwazi eneo jingine la nyuma. Wakati Emmanuel Okwi na Meddie Kagere wao huwalazimisha mabeki kutengeneza uwazi kwa kukimbia nyuma ya mabeki. Unapokimbia nyuma ya mabeki , mabeki huwa na kazi mbili.
Kazi ya kwanza ni kukuangalia mshambuliaji na kazi ya pili ni kutazama mpira, hiki kitu huwafanya mabeki kupoteza uelekeo na mwisho wa siku hujikuta wanatengeneza uwazi, mfano goli la Al Alhly Meddie Kagere alikuwa amekaa nyuma ya mabeki, mabeki wa Al Alhly wakawa na kazi mbili, ya kwanza kumtaza Meddie Kagere kupitia bega lao na kazi ya pili ni kutazama mpira kitu ambacho kiliwasababishia wakose uelekeo na Meddie Kagere kufunga.
MIJONGEO WAKATI TIMU HAINA MPIRA.
Hapa Meddie Kagere anawazidi kina John Bocco na Emmanuel Okwi. Meddie Kagere anakimbia sana wakati akiwa hana mpira kuzidi wote.
KUKABIA JUU (HIGH PRESSING)
Meddie Kagere na John Bocco wanamzidi Emmanuel Okwi kwenye hili. Mfano kwenye mechi dhidi ya Al Alhly, Meddie Kagere na John Bocco walikuwa wanakabia juu sana na kuwafanya mabeki wa Al Alhly wasiwe na uwezo wa kuanzisha mashambulizi.
KUPIGA MASHUTI
Hapa bila shaka wote huwa wanapiga mashuti, lakini Emmanuel Okwi anakiwango kikubwa cha kupiga mashuti kuliko wote. Mfano kwenye mechi dhidi ya Al Alhly yeye alikuwa na mashuti 3 mengi kuzidi John Bocco na Meddie Kagere.
FREEKICK
Emmanuel Okwi ni bora zaidi kwenye eneo hili kuzidi wote . Huwa anapiga freekick ambazo huzaa magoli kuzidi Meddie Kagere na John Bocco.
FOOTWORK
Kwenye eneo hili John Bocco na Emmanuel Okwi wako vizuri zaidi kuliko Meddie Kagere.
NGUVU
Wakati Emmanuel Okwi na John Bocco hujivunia Footwork, Meddie Kagere yeye hujivunia zaidi kwenye eneo la nguvu ya mwili. Yeye huwazidi mabeki kwa kutumia nguvu ya mwili wake.
ONE AGAINST ONE
Okwi ni mzuri akiwa na beki mmoja Kagere pia anaweza kumpita beki akiwa mmoja lakini John Bocco ni ngumu kwake.
HITIMISHO
Kwanini kocha wa Simba hupenda kuwatumia wote watatu kwa wakati mmoja? Kila mmoja huwa anaumuhimu wake , umuhimu ambao huwa na msaada kwenye timu, na umuhimu huu wa kila mmoja huziba udhaifu wa kila mmoja.