Kiungo “Maestro” wa Simba Jonas Gerald Mkude hatokuepo katika mchezo wa mwisho wa kundi D dhidi ya AS Vita ambao ni muhimu kwa Simba ili kuweza kufuzu hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Africa. Hii ni kutokana na kuonyeshwa kadi ya njano katika mchezo dhidi ya JS Saoura ugenini.
Kwa sasa kwenye mfumo wa klabu ya Simba Jonas Mkude ni kama roho katika timu haswa katika eneo la katikati ya uwanja. Kukosekana kwake kutokana na kutumikia adhabu kwa namna moja au nyingine itakua ni pigo kwa vijana wa Patrick Auseems katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya AS Vita ambao msemaji wa Simba ameuita mchezo huo “DO or DIE”
Hakuna shaka Simba ndio nyumbani kwa viungo, kwa maana Simba haijawahi kua na uhaba wa viungo tangu kipindi cha nyuma enzi za kina Selemani Matola, Nicco Nyagawa, Henry Joseph, Haruna Moshi na Jerry Santo mpaka sasa wakiwapo kikosini kina Said Ndemla, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Mohamed Ibrahim “MO”.
Je mwalimu Patrick Auseems atamuandaa nani kwenda kuziba kwa ufasaha nafasi ya Jonas Mkude ili kuiondosha AS Vita?
Je tumtegemee swaiba wake Said Hamis Ndemla kupewa eneo la kati na kulitendea haki? Ama kiungo fundi Mnyarwanda Haruna Niyonzima anaweza akafitii a kuweza kuonyesha vitu vyake mbele ya Wacongo?
Tuamini katika kiwango bora kutoka kwa Hassan Dilunga “HD” ndie atakaeweza kuziba nafasi ya Mkude? Au kiungo mgumu Mzamiru Yassin anaweza kuiongoza Simba katika kuandika historia mpya?