Sambaza....

Leo kuna mechi ambayo inashika hisia za watu wengi wapenda mpira duniani.

Mechi hii inakutanisha timu ambazo zinaonekana bora kwa sasa katika ligi kuu ya England, na ndizo timu ambazo zinaongoza mbio za ubingwa wa ligi kuu ya England.

Manchester City akiwa anaongoza kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Manchester City, hii ndiyo sababu ya kwanza kwa mechi hii kufuatiliwa kwa ukubwa na watu wengi.

Pep Guardiola na Jose Mourinho wamekuwa makocha ambao wana upinzani mkubwa, upinzani unaojenga sababu ya pili kwa mechi hii kufuatiliwa sana kwa kiasi kikubwa.

Katika maisha yao ya kufundisha mpira wamekutana mara 19 ambapo Pep amefanikiwa kushinda mechi 9 dhidi ya 4 za Jose Mourinho huku wakiwa wametoka sare michezo 6 na Jose kufungwa goli 30 huku yeye akifunga goli 19, ambapo Pep Guardiola akipata clean sheets 6 na Jose Mourinho akipata clean sheets 4.

Image result for manchester united vs manchester city

Katika msimu huu Manchester City kashinda mechi 7 zote walizocheza ugenini, wakati Manchester United akishinda mechi zote alizocheza nyumbani. Na leo wanakutana nyumbani kwa Manchester United, sehemu ambayo Manchester United imekuwa sehemu salama kwake kwa sababu mpaka sasa ana mechi 41 hajafungwa kwenye uwanja wake, huku Manchester City ameshinda mechi 7 za ugenini msimu huu.

Kipi kimekuwa mhimili wa Manchester City ?

Wengi watamtaja Kevin De Bryune kama mchezaji mhimili zaidi katika kikosi hiki akifuatiwa na David Silva.

Lakini anasahulika Fernandinho ambaye amekuwa mhimili katika kupata mipira kuanzia eneo la nyuma na katikati kisha kuanzisha mashambulizi.

Yeye ndiye ambaye amekuwa akiwa wafanya kina Kevin De Bryune na David Silva wawe huru na wacheze bila presha yoyote kwa sababu mapishi yote yanaanzia kwake.

Manchester United wanatakiwa wawe makini zaidi na Fernandinho?

Ni ukweli usiopingika Kevin De Bryune na David Silva ndiyo wachezaji wabunifu katika utengenezaji wa magoli, lakini ƴutengenezaji wao wa magoli hauwezi kuwa na nguvu kubwa kama Fernandinho hatokuwa huru kuwapelekea mipira, kumfanya Fernandinho asiwe huru kutamfanya Kevin De Bryune pamoja na David Silva kushuka chini kufuata mipira, hali ambayo itapunguza ufanisi wao.

Image result for manchester united vs manchester city

Manchester United wanatakiwa waweke viungo wengi wa katikati wenye uwezo wa kukaba, hali ambayo itakuwa inawasaidia pia kipindi ambacho Kevin na David Silva watakaposhuka chini.

Hivo yupi ni mtu sahihi kati ya Fellain na Herrera katika mechi hii??

Fellain anakosa match fitness kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo kwa sababu ya majeraha, hivo itakuwa vizuri kwake kutumika kama plan B ya kikosi cha Manchester United.

Hivo Matic na Herrera wapate nafasi katika kikosi cha kwanza, kwa sababu kwa kiasi kikubwa ni wazuri katika kukaba.

Lingard ana nafasi kubwa ya kuanza katika hii mechi?

Jibu ni ndiyo kwa sababu, katika mechi ambazo Manchester United hukutana na timu ambazo zinamiliki mpira, mtu kama Henrink Mickhtryian anakuwa anacheza katika kiwango cha kawaida.

Hivo anahitajika mtu ambaye ni mzuri wakati timu ikiwa na mpira na wakati ambao timu haina mpira.

Uwepo Lingard utakuwa na nafasi kwake yeye kushuka mpaka katikati ya uwanja ili kuongeza idadi ya wachezaji wa katikati ya uwanja, hivo kufanya kuwa 3v3.

Ni Rashford au Martial anayetakiwa kuanza?

Martial ameonekana ana madhara ya moja kwa moja msimu huu kuzidi Rashford linapokuja suala la takwimu za kushambulia lakini katika takwimu za kuzuia amekuwa siyo mzuri sana.

Katika mechi hii ambayo Manchester United kwa kiasi kikubwa itakaa nyuma ya mpira kwa sababu ya aina ya mpira wa Manchester City ambao humiliki mpira zaidi.

Hivo kumwanzisha Rashford kutakuwa na msaada katika kukaba kuanzia kukabia juu mpaka chini, na kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza.

Sambaza....